IQNA

Vipindi vya Qur'ani Tukufu  katika msikiti mkuu wa Makka Vilihudhuriwa  zaidi ya watu 210,000 Mwaka Jana 

17:05 - January 30, 2025
Habari ID: 3480127
IQNA - Programu za Qur'an zilizoandaliwa katika Msikiti mkuu wa jiji tukufu  la Makka zilihudhuriwa na zaidi ya mahujaji na waumini 210,000 mwaka 2024.

Zaidi ya Watu 210,848 Wafaidika na Vipindi vya Usomaji na Kuhifadhi Qur’ani  katika Msikiti Mkuu wa Makka.

Jumla ya wanaume na wanawake 210,848 walinufaika na vipindi vya usomaji na kuhifadhi Qur’ani vilivyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Makka, eneo takatifu zaidi katika Uislamu, mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu rasmi.

 Idadi ya vipindi hivi ilifikia 75,190, ambavyo vilifanyika kwa jumla ya saa 48,678, kulingana na taarifa ya Urais wa Masuala ya Kidini katika Misikiti Miwili Mitukufu.

 Vipindi hivyo vilihusisha kozi za kawaida, kozi za mtandaoni, na kozi za wageni, huku ratiba tofauti zikiandaliwa kwa wanaume na wanawake. Vipindi vya kuhifadhi Qur’ani  viliendeshwa na wataalamu 213 wa usomaji wa Qur’ani Tukufu.

 Taasisi ya serikali ilieleza kuwa kozi hizi zimeandaliwa ili kuwawezesha waumini na wageni kujifunza usomaji na uhifadhi wa Qur’ani  kwa usahihi kwa kutumia mbinu madhubuti za kielimu.

 Mamilioni ya Waislamu kutoka kote ulimwenguni hufurika katika Msikiti Mkuu wa Makka  ili kutekeleza ibada ya Hijja na Umrah. 

 Hijja, ambayo ni miongoni mwa nguzo za Uislamu, ni ibada inayowalazimu Waislamu wote walio na uwezo wa kimwili na kifedha kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yao.

 Takriban mahujaji milioni 1.8, wakiwemo milioni 1.6 kutoka nje ya Saudi Arabia, walitekeleza ibada ya Hija mwaka jana. Maandalizi yanaendelea kwa msimu ujao wa Hijja.

 Baada ya kutekeleza ibada ya Hija na Umrah, mahujaji wengi huenda Madina kuswali katika Msikiti wa Mtume, ambao ni msikiti wa pili mtakatifu zaidi katika Uislamu.

 

/3491662

 

 

captcha